Mabingwa wa ligi kuu Vodacom Young Africans na timu zinginezo zilishoriki ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha 2015/16 watakabidhiwa zawadi zao na kampuni hiyo ya mawasiliano mwezi ujao.
Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu alisema ucheleweshwaji wa zawadi umetokana na baadhi ya timu kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika na shughuli za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
"Tunaomba radhi kwa wahusika, wachezaji na wadau wa soka kwa kucheleweshwa kwa zoezi hili ila tunawahakikishia zawadi ziko tayari na zitatolewa mwezi ujao." Alisema meneja huyo
Pia Nkurlu alitoa shukurani kwa wadau wote waliofanikisha ligi hiyo lakini aliomba kujitokeza kwa wadhamini kwa ajili ya kuinyanyua zaidi ligi kuu kwani changamoto bado ni nyingi ikiwemo namna ya kuwawezesha wachezaji wanufaike na ushiriki wao kwenye ligi.
Hata hivyo aliongeza kuwa Vodacom itaendelea na udhamini wa ligi hiyo hadi itakapomaliza mkataba na wake na TFF.

Comments
Post a Comment