Mwenyekiti wa timu ya West Ham united ya England David Sullivan amesema kuwa nyota wa timu hiyo Dimitri Payet hauzwi kwa dau lolote lile.
Payet ambaye alifunga goli la ushindi na kuibeba Ufaransa katika mchezo wa ufunguzi dhidi Romania ameanza kunyatiwa na baadhi ya timu kubwa ulaya ambazo zinahitaji huduma ya mcheza huyo mwenye kiwango cha hali ya juu.
"West Ham ipo kwenye mipango mizito ya kuimarisha na kujenga timu bora na payet ni mchezaji muhimu kwetu.
"Jambo la rahisi ni kwamba mchezaji huyo Hauzwi kwa Gharama yoyote ile." Aliongeza Sullivain.
Payet 29, amekuwa moto wa kuotelea mbali tangu atue kwa wagonga nyundo hao wa London na sasa amekuwa mchezaji tegemezi kwenye timu ya taifa ya Ufaransa.

Comments
Post a Comment