Timu ya Yanga leo imejaza idadi kubwa ya mashabiki wao ambao wamejitokeza kwa wingi kuisapoti timu hiyo dhidi ya TP mazembe.
Mapema leo tangu asubuhi mashabiki walionekana wamekusanyika kwa wing kujaza majukwaa ya uwanja wa taifa huku wakisubiri kwa hamu mtanange huo.
Yanga kupitia msemaji Jerry Muro ilitangaza kufuta viingilio kwa mashabiki ili waweze kufika kwa wingi kushuhudia pambano hilo la nyumbani.
Yanga inacheza mchezo wa pili kwenye hatua ya makundi baada ya kupoteza ule wa kwanza dhidi ya MO Bejaia na kwa muda wote waliweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi.
Comments
Post a Comment