Yanga yapaa Uturuki, yamwacha Juma Abdul


Timu ya imekwea pipa kuelekea nchini Uturuki kuweka kambi maalum ili kujiandaa na mechi ya MO Bejaia ya nchini Algeria.

Katika safari hiyo Yanga imemwacha beki wake kisiki Juma Abdul ambaye atakaa nje wiki mbili kutokana na majeraha.

Yanga inajipanga vilivyo ili waweze kuwa nondo kabla ya kushuka dimbani dhidi ya MO Bejaia Juni 19 mwaka huu.

Wengine waliochwa ni pamoja na Malimi Busungu ambaye ni majeruhi, Salumu Terera ambaye hajaongezewa mkataba mpya, Benedicto Tinocco na Paul Nonga ambao hawapo kwenye programu ya mwalimu Hans Pluijm.

Comments