Timu ya Yanga leo imepoteza pointi 3 kwa mara ya pili baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa TP Mazembe kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walishindwa kutengeneza nafasi za magori ambapo kipindi cha pili mazembe warirudi na makakati mwingine na kuweza kupata goli la ushindi.
Bao la TP Mazembe lilifungwa na Merveille Bope kunako dakika ya 74 ya mchezo baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa baada Thomas Ulimwengu kufanyiwa madhambi na Kevin Yondani.
Yanga ina kibarua cha kuchuana na Medeama ya Ghana katika mchezo utakochezwa kwenye uwanja wa taifa ikiwa bado ina nafasi ya kuvuka kwenye hatua ya nusu ya fainali endapo itashinda mechi zote.

Comments
Post a Comment