Kiungo wa Napoli Piotr Zielinsk ameweka wazi kuwa anataka kujiunga na liverpool licha ya kufukuziwa na timu kadhaa.
Raisi wa timu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amesema kuwa licha ya kutaka kumpa mkataba wa kudumu kiungo huyo wa Empoli ambaye pia anafukuziwa na Dortmund, raisi ameweka wazi kuwa mchezaji huyo anaitaka Liverpool.
Klopp anataka kuimarisha sehemu ya kuingo katika timu yake na mchezaji amekuwa moja ya wachezaji muhimu anaowahitaji kwenye timu yake msimu huu.
"Tunaangalia uwezekano wa kumsajili Fabinho kutoka Monaco kama mbadala wa Zielinski ambaye tulijaribu kuzungumza na familia yake lakini alikataa mpango wa kubaki napoli." Alisema raisi huyo

Comments
Post a Comment