Ame Ali kuziba pengo la kiiza Simba


Timu ya Simba imefikia pazuri katika suala la kupata mrithi wa Hamis kiiza kutokana na dili la usajili wa Ame Ali kwenda vizuri.

Simba iliachana kiiza lakini sasa imejipanga kumng'oa Ame Ali kutoka Azam ili kuiweka sawa safu yake ya ushambuliaji.

Mazungumzo baina ya Simba na Azam yanaendelea vizuri na huenda Ame Ali aliyebakiza mwaka mmoja kwenye timu yake akatua msimbazi muda wowote kuanzia sasa.

Ame Ali Ally aling'ara akiwa na Mtibwa msimu wa 2014/15 ambapo Azam ilimtolea macho na kumsajili nyota huyo.

Comments