Azam kujipima nguvu na ashanti


Timu ya Azam itashuka dimbani siku ya jumapili katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Ashanti united.

Kocha mpya wa timu ya Azam Mhaspaniola Zeben Hernandez aliomba uongozi wa timu hiyo umtafutie mechi moja ya kirafiki ili kupima nguvu kikosi chake baada ya wiki moja ya mafunzo.

"Vijana wameonesha utayari mazoezi lakini haliwezi kunipa uhakika sana nahitaji mechi ya kirafiki kupima kikosi changu." Alisema Hernandez

Tayari uongozi wa Azam umefanikiwa katika hilo baada ya kufanya makubaliano na Ashanti united ambao kwa upande wao watatumia nafasi hiyo kujipima nguvu kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la kwanza.


Comments