Azam yaanza vizuri majaribio


Timu ya Azam FC imeonesha iko njema chini ya kocha kijana Zeben Hernandez baada ya kuichapa Ashanti bao 2-0.

Mchezo huo wa kujipima nguvu ulichezwa leo katika uwanja wa Azam, Chamanzi Complex ambapo soka maridadi limeoneshwa na timu Hiyo.

Azam ilifunga magoli hayo kipindi cha pili kupitia Mudathir Yahya dakika ya 69 na Masoud Abdallah aliyefunga bao la pili.

Comments