Timu ya Azam imechoshwa na mivutano dhidi ya mshambuliaji wao Kipre Herman Tchetche na sasa wameamua kumwacha aende anakotaka.
Licha ya mchezaji huyo kubakiza mwaka mmoja na Azam lakini ameshindwa kutimba kambini mpaka sasa na kuna uvumi Yanga ni moja kati ya timu zinamfukuzia mchezaji huyo.
Kipre yupo Oman kwa sasa akiendelea kufanya mazungumzo na moja ya timu ambazo Azam haikuweka wazi jina lake huenda kiasi cha pesa kikatumwa wakati wowote Azam.
Moja wa viongoz wa Azam alisema kuwa mchezaji huyo hatauzwa chini ya Tsh milioni 322 kwa sababu kwa kuwa kiwango hicho ni kikubwa kwa timu zetu za ndani.

Comments
Post a Comment