Balotelli ajifua na Academy ya Liverpool


Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameamua kujifua na timu ya vijana ya Liverpool katika harakati za kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu England.

Liverpool haikuungana na Mario Balotelli katika ziara zake za soka, kutokana mchezaji huyo kuwa nje ya mipango ya Kocha Jurgen Klopp ambaye alimwambia anaweza kutafuta nje ya Liverpool nakuondoka.

Balotelli alionekana katika picha ya pamoja aliyopiga na vijana hao wa Liverpool katika Academy hiyo mara baada ya mazoezi na kuiposti picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram.

Balotelli ambaye alishindwa kung'ara na Liverpool alipelekwa AC Milan kwa mkopo lakini hata hivyo hakuweza kufanya vizuri jambo lilipolekea timu hiyo kumrejesha kwenye timu yake.

Picha na Daily Mail

Comments