Beki mpya mbioni kutua Liverpool


Liverpool iko mbioni kukamilisha usajili wa beki wa kati Ragnar Klavan kutoka FC Augsburg ya Ujermani.

Liverpool imeweka mezani dau la Euro 4.5 milioni kama ada ya uhamisho wa mchazaji huyo ambaye timu ya Liverpool ilichuana nae timu hizo zilipokutana kwenye michuano ya Europa ligi kwenye hatua ya mtoano.

Liverpool inataka kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi baada ya kuondoka kwa Kolo Toure na kuumia goti kwa Mamadou Sakho  ambaye atakosa mechi za awali ligi itakapoanza.

Kama usajili wa mchezaji huyo utakamilika Klavan 30, atakua mchezaji wa pili kutoka nchini Estonia kucheza katika ligi ya EPL baada ya kufanya kwa aliyekuwa kipa wa zamani wa Derby County na Arsenal Mart Poom.

Comments