Chama cha soka England kimempitisha aliyekuwa kocha
wa muda wa timu ya Sunderland Sam Allardyse ‘Big Sam’ kuwa kocha wa timu ya
taifa ya Uingereza.
Kocha huyo wa zamani wa Bolton na West Ham huenda
akatangazwa rasmi muda kuanzia sasa kuwa ndiye mrithi wa kiti cha aiyekuwa
kocha wa England Roy Hogdson.
Roy Hodson alioneshwa mlango wa kutokea baada ya England kufanya vibaya kwenye michuano ya UEFA Euro iliyofanyika nchini Ufaransa ambapo timu hiyo iliondolewa na Ice land kwenye hatua ya 16 bora

Comments
Post a Comment