Timu ya Chelsea imeibuka kifua mbele jijin California baada ya kuilaza Liverpool kwa kuifunga goli 1-0 katika michuano ya mabingwa kimataifa.
Chelsea ilipata bao hilo kupitia Gary Cahil aliyefunga kwa kichwa kunako dakika ya 10 ya mchezo baada ya kuunganisha mpira wa kona.
Licha ya Cesc Fabrigas kulimwa kadi nyekundu lakini Chelsea iliweza kuhimili kwa dakika zote 90 na kutoka kifua mbele kwa ushindi huo dhidi ya Liverpool.
Matokeo ya mechi zilizochezwa kwenye michuano hiyo ni Real Madrid 1-3 PSG na AC Milan 3-3 Bayern Munich ambapo Milan wamevuka baada ya kuinyuka Bayern Mubich kwa mikwaju ya Penati,

Comments
Post a Comment