Timu ya Chelsea imekubali kulipa dau la £ 32 milioni kama ada ya uhamisho wa kiungo N'golo Kante kutoka Leicester city.
Taarifa kutoka Sky kutoka Sky sports ya Uingereza zimethibisha kuwa mchezaji huyo yupo kwenye mazungumzo na timu ya Chelsea baada ya makubaliano ya ada ya uhamisho.
Licha ya Kante kupiganiwa na timu nyingi lakini hadi sasa ni timu ya Chelsea pekee ndiyo inayoongoza kwenye mbio za kumwania kiungo huyo ambaye huenda akatua Chelsea muda wowote kuanzia sasa.
Kuna taarifa pia kuondoka kwa mchezaji huyo kunamfanya Riyad Mahrez ambaye ni mchezaji mwenza na Kante Leicester city kuonesha dalili za kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kukataa ofa ya mshahara wa £ 100,000 aliyopewa na timu yake.
Comments
Post a Comment