Beki wa Manchester city Gael Clichy amesema ni kosa kubwa kula misosi isiyofaa chini ya kocha Pep Gurdiola.
Clichy alisema Gurdiola hataki uzito wa juu kwa wachezaji wake na kushindwa kufanya vizuri katika msimu mpya wa ligi.
"Gurdiola amekataza vyakula vinavyonenepesha ikiwemo Juice na pizza, tunakiwa kuwa na afya kwa ajili ya mashindano." Alisema Clichy.
"Kama huwezi kujitunza kwa Gurdiola, basi ni makosa makubwa, hautakuwa sehemu ya timu, ametuzuia kuwa wazito." Aliongeza Clichy

Comments
Post a Comment