Mwenyekiti wa timu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge a mesema timu ya Borrusia Dortmund inataka kumrudisha kiungo wao wa zamani Mario Gotze.
Gotze 24, aliondoka Dortmund miaka 3 iliyopita lakini tangu atue Allianz Arena amekosa namba ya kudumu kwenye timu hiyo ambayo imesheheni nyota kadhaa wenye majina.
Kulingana na mwenyekiti huyo wa Bayern huenda dili la mchezaji huyo kurudi Dortmund likatiki muda wowote kuanzia sasa kutokana na mazungumzo kwenda vizuri.
Gotze alipewa asilimia kubwa za kujiunga na timu ya Liverpool kutokana na aliyekuwa kocha wake katika timu ya Dortmund Jurgen Klopp kuinoa Liverpool lakini hata Gotze alikataa

Comments
Post a Comment