Fergie: Mourinho kufanya makubwa Man united


Aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Manchester united Sir Alex Ferguson amesema kuwa anaona mabadiliko makubwa kwenye timu hiyo chini ya Mourinho.

Ferguson alisema timu ya Manchester united itafanya mambo makubwa chini ya Mreno huyo ambaye amewahi kupata mafanikio mbali mbali alipokuwa na timu ya Porto, chelsea, Intermilan na Real Madrid.

"Nadhani kuna mambo makubwa zaidi yanaenda kutokea Manchester united."  Alisisitiza Ferguson

"Amepata mataji ya klabu bingwa Ulaya mara mbili akiwa na timu tofauti na kila alipofundisha hakukosa ubingwa wa ligi" Aliongeza Sir Alex Ferguson

Mourinho alifanya mkutano wake wa kwanza jana tangu atue Man united na kuhaidi kuwa anahitaji kusajili wachezaji wengine kuimarisha timu hiyo.

Comments