Genk ya Samatta mbele kwa mbele Europa


Klabu ya KRC GENK ya Belgium inayochezea mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta. Imeandikisha ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kwanza wa raundi ya tatu kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya Europa.

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Leon Bailey dakika ya 31 kipindi cha kwanza kwa shuti kali la nje ya boksi la kumi na nane na mpira ukatinga wavuni.

Mbwana Samatta na Bailey walipiga mashuti mengine kadhaa wakijitahidi kuipatia timu yao goli lingine lakini kipa wa Cork City, McNulty alikuwa imara langoni mwake!!

KRC Genk itarudiana na Cork City alhamisi ijayo nyumbani kwa Cork city nchini Ireland na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi.

Comments