Timu ya Genk imesonga mbele baada ya kuing'oa Buducnost ya Romania kwa mikwaju ya Penati 4-2 baada kufika dakika 120 za mchezo.
Samatta alifunga katika mchezo wa kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-0 waliopata nyumbani lakini jana mambo yalikuwa tofauti baada ya Genk kipigo cha mabao 2-0.
Hata hivyo mechi hiyo ilifika hadi kwenye matuta baada ya kila timu kushindwa kutikisa nyavu za mwenzake katika dakika 30 za nyongeza na Genk ilishinda kwa mikwaju 4-2 ukiwemo ule aliofunga mtanzania Mbwana Samatta.

Comments
Post a Comment