Gomes atua Barcelona


Timu ya Barcelona imefanikiwa kumnasa kiungo wa timu ya Valencia Andre Gomes kwa dau la £50 milioni.

Barcelona imeipiku Real Madrid kwenye vita ya  kumng'oa mreno huyo Valencia ambaye alikuwamo kwenye kikosi cha Ureno kilichotwaa taji la UEFA Euro mwaka huu.

Andre Gomes anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Barcelona msimu huu baada ya Ule wa mabeki wawili kutoka nchini Ufaransa.

Comments