Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola amesema kuwa atamsalimia kocha Jose Mourinho pindi timu hizo zitakapokutana.
Gurdiola na Mourinho hawakuwa kwenye mahusiano mazuri walipokuwa premiera la Liga ambapo vita ya Maneno iljengeka kati yao.
"Kwanini nisimsalimie, tutakapokutana lazma tusalimiane na tutashikana mikono." Alisema Gurdiola
Mahasimu hao wawili waliwahi kuwa na vita ya maneo wakati Gurdiola akiwa na Barcelona na Mourinho akiwa Real Madrid.
Lakini sasa mahasimu hao wanakutana tena England wakiwa kwenye timu zenye upinzani mkali katika jiji la Manchester.

Comments
Post a Comment