Hakuna ubaya Vicent Bossou kuibuka shujaa Yanga


Wakati Yanga ikipambana na Medeama katika mchezo wa marudiano nchini Ghana, jicho langu lilikua sehemu ya kiungo cha Yanga. Licha ya kwamba kuna uhakika wa kazi nzuri ya Thabani Kamusoko pamoja Haruna Niyonzima nilikosa imani na Mbuyu Twitte.

Yanga inaonesha wazi inashida na kiungo wa kukaba, wengi hawaelewi. Sehemu hiyo ndiyo nguzo ya timu yaan kuanzia kuzuia na kuongoza mashambulizi, endapo timu ikisukwa vizuri eneo hilo basi bila shaka mambo huenda vizuri kunako safu ya kiungo.

Unaweza ukacheka lakini si mambo ya kuchekesha inabidi kusikitika na kuhuzunika, mara nyingi huwa najua na kutambua beki zetu hapa Tanzania hukosa hukosa umakini. Kilichotokea kati ya Yanga na Medeama ni vituko.

Licha ya Yanga kukosa kiungo kwa kuongoza na kutuliza mashambulizi, nadhani beki ya kati iligharimu zaidi timu hiyo, kilichofanywa na Nadir Haroub pamoja Kevin Yondani ni vitu vya kusikitisha.

Medeama hawakutumia nguvu nyingi kupata ushindi kwa namna nyingine ni kuwa Yanga iliruhusu magoli mepesi au rahisi kutokana na beki ya kati kucheza vibaya.
Walichokifanya Medeama ni kusoma saikolojia ya ile beki ya Yanga, goli la pili lilionesha ni jinsi gani Medeama walivyosoma ubovu wa Safu ile ya ulinzi.

Kutokana na matokeo ya mechi ile wingi wa mashabiki wa Yanga wanamkumbuka shujaa anayevuma kimya kimya kwenye timu hiyo Vicent Bossou. Nadhani kuna haja ya Cannavaro na Yondani kumpumzika.

Nadhani ipo haja ya Kevin Yondani na Cannavaro kuongozwa na Vicent nikiwa na maana kuwa ni lazma mwalimu afanye maamuzi mmoja kati dhidi ya Vicent Bossou.
Wengi walidhani kulikuwa na afadhali ya kutolewa kwa Yondani na kuingia kwa Dante. Lakini bado kulikuwa kuna hatari kwa kuwa beki wa mwisho ambaye ni  Nadir Cannavaro alikosa utulivu, mahesabu na maamuzi sahihi.

Vicent Bossou ni tofauti kidogo, raia huyu wa Togo ni mtulivu na mwenye mahesabu ya hali ya juu katika kuahirisha tatizo kwenye safu ya ulinzi nadhani Watanzania walichelewa kumwelewa na sasa umuhimu wake umeonekana endapo atakakosekana uwanjani.

Wazungu wanasema 'from zero to hero', wakiwa na maana kuwa kutoka sifuri hadi shujaa,  watu walidhania hakuna kitu kwa Bossou nadhani leo ni shujaa kwa wana Yanga.

Wenye kuona mbali waliona kitu kwa beki ambaye ana uhakika wa namba kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo, kama mchezaji hapotezi namba timu ya taifa basi hilo ni jembe.

Hakuna ubaya wa bossou kuwa shujaa hata kama ni mgeni, Medeama imeleta sura na mtazamo mpya kwa Kevin Yondan na Cannavaro, nadhani bao 3-1 zilikuwa chache kulinganisha na kiwango kibovu kilichooneshwa na beki ya Yanga.

Comments