Safari ya Afisa mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba nchini Ghana ni katika suala zima la kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Medeama Kwame Boahene.
Azam inataka kuachana na Kipre Tchetche ambaye anasumbua uongozi wa timu na badala yake wamehamisha majeshi yao kwa nyota huyo wa Medeama.
Mipango ya Azam kumfuatilia mchezaji huyo ilianzia Tanzania katika mchezo ambao Medeama ilitua ugenini kuikabili Yanga katika mchezo wa makundi uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Bosi huyo alitua Ghana akiwa kwenye mipango mizito ya kufanikisha usajili wa Strika huyo ambaye alianza kumfuatilia mazoezini na baadae katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Medeama ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-1.

Comments
Post a Comment