Winga wa Liverpool Jordon Ibe huena akatua katika timu ya Bournemouth muda wowote kuanzia sasa baada ya zoezi lake la uhamisho kuelekea ukingoni.
Liverpool imekubali dau la euro 15 milioni na kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo abaye ni raia wa Nigeria na huenda mchezaji huyo akatua kwenye timu hiyo.
Klopp amemsajili baadhi ya nyota akiwemo Sadio Mane na yupo kwenye mipango ya kukamilisha usajili wa wachezaji wengine muhimu anaona ni vema kumuuza Ibe.
Jordon Ibe ni moja kati ya wachezaji makinda ambao waliwahi kupewa nafasi ya kujulikana kwenye ulimwengu wa soka na kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers ambaye kwa sasa yupo Celtic ya Scotland

Comments
Post a Comment