Licha ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha mwalimu Zinedine Zidane kiungo James Rodriquez amegoma kuondoka Bernabeu.
Raia huyo wa Colombia amesema licha ya baadhi ya timu kutoa ofa kubwa Bernabeu yeye binafsi haoni sababu ya kuondoka kwenye timu hiyo.
"Nadhani uhimisho wa £ 85 milioni ni heshima kwangu lakini sitaki kuondoka Real Madrid." Alisema Rodriquez
Kwa upande wa kocha wa Timu hiyo Zinedine Zidane amesema kuwa James ana nafasi kubwa ya kuonesha uwezo wake na kupata namba kwenye timu hiyo.

Comments
Post a Comment