Kocha wa timu ya Mwadui ya Shinyanga Jamuhuri Kiwehlo 'Julio' amesema njaa ndizo zinazojaza wachezaji wa kigeni Tanzania.
Julio alisema wachezaji wengi wa kigeni hawana viwango bora wengi wao wanaganga njaa kutafuta maisha katika soka la Tanzania huku akisisitiza hana mipango ya kusajili wachezaji wa kigeni.
Kocha huyo aliongeza kuwa mipango yake kwa sasa ni kusajili wachezaji ndani ya Tanzania kwa kuwa kuna vipaji vya kutosha ili kufanikisha usajili usajili wa wachezaji 23 wakimemo wachezaji 20 wa ndani na magoli kipa 3.
"Wachezaji wa kigeni wenye hadhi kimataifa hapa Tanzania ni Donald Ngoma (Yanga), Kipre Tchetche (Azam) na Pascal Sergi Wawa lakini hao wengine wote wanaganga njaa." Alisema Julio.

Comments
Post a Comment