Beki wa kulia wa timu ya Yanga ndiye mwanasoka bora wa ligi kuu baada ya kushinda tuzo hiyo jana.
Juma Abdul ndiye aliyepata kura nyingi kutokana na kiwango bora alichokionesha msimu uliopita kwenye ligi kuu ya Vodacom huku pasi na krosi zake nyingi zimekiwa zimeongoza ushindi wa Yanga katika msimu wa ligi kuu ulioisha.
Mbali na tuzo hiyo Mohamed Hussein wa Simba ndiye aliyeibuka mchezaji bora chipukiz wa Msimu, Thabani Kamusoka ndiye mchezaji bora wa kigeni ligi kuu na Ibrahimu Ajib wa Simba ndiye mfungaji bora wa goli la msimu ligi kuu.
Pia kwa upande wa makocha Hans Pluijm wa Yanga ndiye aliyeibuka mshindi wa tuzo ya kocha bora ligi kuu, huku tuzo ya timu bora ligi kuu ikitua kwa Yanga ambao ndiyo mabingwa 2015-16.
Hata hivyo timu ya Mtibwa ndiyo ndiyo timu yenye zaidi ligi kuu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo jana.

Comments
Post a Comment