Kante 25, amesaini mkataba wa miaka 5 na sasa ni mchezaji halali wa Chelsea ambapo ataanza kitumikia timu hiyo muda wowote kuanzia sasa.
Kante anakuwa mchezaji wa pili kusaini Chelsea baada Michy Batshuay kufanya hivyo baada ya kufanyiwa vipimo jijini Bordeaux na daktari wa Chelsea wakati timu ya Ubelgiji ikiendelea kusonga mbele katika fainali za UEFA Euro nchini Ufaransa.
Kuondoka kwa Kante kunafungua milango kwa Rihad Mahrez ambaye naye anataka kutimka kutafuta maisha kwenye moja ya timu kubwa barani Ulaya.

Comments
Post a Comment