Kiungo mpya wa timu ya Chelsea N'golo Kante amesema kuwa hotuba iliyotolewa na kocha wa Chelsea Antonio Conte ndiyo imemshawishi kutua Stamford Bridge.
Kante 25, ambaye aliyekuwemo kwenye kikosi cha ufaransa kwenye michuanao ya UEFA Euro alisema kuwa mambo na ndoto alizoziongelea Conte ni mambo ambayo yalikuwa kwenye mipango yake hivyo hakuona sababu ya kumzuia yeye asitueChelsea.
"Ni klabu kubwa iliyoajiri kocha mkubwa ambaye atatimiza ndoto zangu, mipango ya timu na hotuba ya mwalimu Antonio Conte imenishawishi kutua Chelsea.
"Nasubiri kuitumikia timu yangu, nijitume na kuiletea mafanikio makubwa." Alisema Kante
Pia mchezaji huyo aliongeza kuwa msimu ulipoita ulikuwa ni wa mafanikio kwake na hautasahaulika licha ya kukosa taji la UEFA Euro kante alisema ni jambo la heshima kwa hatua ambayo Ufaransa ilifika.

Comments
Post a Comment