Kaseja apewa ukocha Serengeti boys


Kipa wa zamani wa timu ya Simba Juma Kaseja kwa sasa ndiye kocha wa makipa wa ya taifa ya vijana 'Serengeti' boys .

Kaseja ataungana na timu hiyo ambayo itaweka kambi yake nchini Madagascar kupitia Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi.

Kipa huyo ambaye alitamba akiwa na Simba alikua kwenye mipango ya ya kuongeza mkataba mpya na timu yake ya sasa Mbeya city.

Kaseja amekaimu nafasi hiyo kutokana kocha aliyekuwepo kuelekea shuleni kundelea na kozi za ukocha zinazoendelea hapa nchini.

Comments