Timu Simba leo itashuka dimbani kwa mara ya kwanza chini ya kocha Joseph Omog dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro.
Simba inaingia dimbani kujipima nguvu na mwalimu Joseph Omog anataka kungalia kama mbinu zake zinafanya kazi.
Simba imejichimbia kambini katika mji Morogoro kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom 2016/17.
Simba ina mechi tatu za kujipima nguvu kabla ya Simba day ikiwemo mechi ya leo, na itarajia pia kushuka dimbani dhidi ya Polisi Morogoro na baadae itarudiana na Burkina Faso nje ya mji huo.

Comments
Post a Comment