schweinsteiger akiwa na kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
Kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger ametangaza kustaafu soka la Timu ya taifa akiwa ameichezea Ujerumani mechi 120.
Mchezaji huyo mwenye umri w miaka 31 ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi wakiwa na kikosi cha Ujerumani, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza michuano ya ulaya Euro 2016, akicheza mechi tano kabla ya timu yake kutolewa na mwenyeji Ufaransa kwenye nusu fainali
Schweinsteiger aliyeanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2004 amestaafu akiwa amechukua kombe ld dunia 2014 baada ya kumpiga Argentina kwenye fainali baada ya mumaliza washindi wa tatu katika michuano hiyo mwaka 2006 na 2010, alivaa medali ya shaba pia mwaka 2008 katika michuano ya Ulaya.
Schweinsteiger ameandika waraka akiitimisha maisha yake ya soka na timu ya Taifa ya Ujerumani

Comments
Post a Comment