Liverpool imekamilisha usajili wa beki Ragnar Klavan baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kwa ada ya uhamamisho wa Euro 4.5 milioni.
Beki huyo kutoka Augsburg ya Ujermani amekabidhiwa jezi namba 17 muda mfupi baada ya kumilisha suala la vipimo na kumwaga wino wa kuitumikia vijogoo hao wa Merseyside.
"Nafurahi kujiunga na Liverpool, ni heshima kubwa kuwa na klabu hii na inashanganza, kwa sababu hii ni moja ya timu bora duniani." Alisema Klavan
"Ni ndoto niliyonayo kwa miaka 22, nilipanga itokee nicheze Uingereza, hii ni ligi yenye mvuto duniani na wachezaji wake, na wachezaji wa hapa wanashangaza pia." Aliongeza Klavan

Comments
Post a Comment