Baada ya kusaini mkataba mpya na Liverpool jurgen Klopp yupo kwenye mpango mzito wa kuandaa Academy mpya.
Klopp alisaini mkataba wa miaka 6 utakaomuweka Liverpool hadi 2022 na sasa anataka kuifanya timu hiyo kuwa zao la vipaji barani Ulaya.
"Tunahitaji kuimarisha klabu, tunahitaji timu yetu iendelee zaidi na isonge mbele hayo ndiyo malengo yetu" Alisema Klopp katika mahojiano na Sky sports
Klopp anahitaji kuona timu hiyo inatoa vipaji kama ilivyokuwa kwa Steven Gerrard, Jamie Carragher na Michael Owen
Comments
Post a Comment