Klopp kuongezewa mkataba Liverpool


Timu ya Liverpool ipo kwenye mipango ya kumuongeza mkataba mpya kocha wa timu Jurgen Klopp.

Licha ya kocha huyo kutumikia mwaka mmoja pekee kwenye timu hiyo lakini mmiliki wa timu ya Liverpool John Henry amevutiwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Klopp atue Anfield.

 Vyanzo vya habari kutoka BBC, Gurdian na Liverpool Echo vimethibitisha Liverpool imepitisha mkakati huo mpya wa kumpatia kocha huyo mkataba mpya hadi 2018 ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine hadi 2019 kulingana na mafanikio atakayoleta kwenye timu hiyo.

Pia Liverpool ipo kwenye mpango wa kumfanya Klopp kuwa kocha anayelipwa zaidi ya Arsene Wenger wa Arsenal na Jose Mourinho wa Manchester united.

Comments