Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa Liverpool ya sasa haifanani na ile iliyoachwa na Brendan Rodgers.
Klopp alisema hakuna shaka juu ya Liverpool ya sasa ambayo inakwenda kufanya vizuri kwenye chini yake huku akisisitiza kuwa hakuna kisingizio cha kushindwa kutokana na usajili uliofanywa na Brendan Rodgers.
Kocha huyo amefanya usajili wa wachezaji ambao wamekuwa chaguo lake akiwemo Sadio Mane, Giorginio Wijnaldum, Ragnar Klavan, Marko Grujic, Joel Matip, Loris Karius na Alexander Manninger.
"Hiki ni kikosi changu sasa." Alisema Klopp, usajili niliofanya sasa ni mapendekezo ya kikosi changu kipya.
"Tutapigania kila kitu yakiwemo mataji yote muhim, hakika nina furaha na kikosi changu hata mashabiki wetu wana furaha pia." Alisema Klopp.

Comments
Post a Comment