Timu ya Leicester city ya Uingereza imevunja rekodi yake ya usajili baada ya kumnasa strika wa CSKA Moscow Ahmed Musa.
Leicester imekamilisha usajili huyo kwa ada ya uhamisho wa euro 15 milioni ikiwa ni kiasi ambacho timu hiyo haijawahi kutumia kwenye usajili,
Musa ambaye ni raia wa Nigeria alifunga magoli 13 na kutengeneza nafasi tano za magoli katika mechi 30 alizocheza akiwa na CSKA Moscow.
Pia mchezaji huyo amefunga jumla ya magoli 11 katika mechi 58 alizoichezea timu ya taifa ya Nigeria.

Comments
Post a Comment