Liverpool yafanya kweli kwa Wijnaldum


Timu ya Liverpool imethibitisha nia yake ya kumng'oa kiungo wa Necwcastle Giorginio Wijnaldum baada ya kuweka mezani dau la Euro milioni 25 kama ada ya uhamisho.

Awali Liverpool ilikuwa ikihusishwa kwenye mipango ya kumng'oa Mario Gotze kutoka Bayern Munich lakini dili hilo lilikwama na sasa Klopp anaona Mholanzi huyo ndiyo mbadala wa usajili wa Gotze.

Newcastle imesema haitamtoa mchezaji huyo chini ya dau la uhamisho wa Euro 27 milioni ingawa mpaka sasa bado timu hizo zinaendelea na mazungumzo.

Inasadikika Liverpool huenda ikawatumia wachezaji wake Jon Flanagan na Lucas Leiva kama sehemu dili la kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Anfield.

Comments