Liverpool yainyonga AC Milan


Timu ya Liverpool imeibuka kifua mbele dhidi Milan baada ya kuichapa timu hiyo bao 2-0.

Liverpool ilipata bao la kwanza kupitia Divock Origi kunako dakika ya 59, huku bao la pili likiwekwa nyavuni na Roberto Firmino wote wakiwa wametokea benchi.

Jurgen Klopp bado anaendelea na zoezi kuimarisha timu hiyo ambapo kulingana na usajili aliofanya kocha amehaidi mambo makubwa msimu ujao.

Liverpool imejiuliza baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Chelsea siku tatu zilizopita baada ya kufungwa bao 1-0 na leo wameibuka vinara.

Comments