Mahadh fiti kuivaa Medeama

Kiungo wa timu ya Yanga Juma Mahadh atakuwa kuwa fiti kuivaa Medeama ya Ghana wiki ijayo.

Mahadh alikuwa anasumbuliwa na nyonga na akashindwa lakini sasa anaendelea vizuri na mazoezi binafsi.

Mchezaji huyo alishindwa kumaliza mechi dhidi ya TP Mazebe baada ya kusumbuliwa na nyonga ambayo imemuweka nje ya Uwanja kwa muda wa wiki mbili sasa.

Mchezaji huyo aliyekuwa mwiba katika mchezo wa Mazembe  alisajiliwa na Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga.

Comments