Timu ya Manchester united imewasili nchini China ikiwa ni moja katika harakati za timu hiyo kujiandaa na ligi kuu nchini England (EPL).
Manchester united iliwasili mapema leo Shanghai bila makamu mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward ambaye ataungana na timu hiyo kwenye michuano ya International champions cup inayofanyika Beijing katika mechi dhidi ya Manchester city weekend hii.
Wachezaji watatu wa Manchester united akiwemo Wayne Rooney, Henrikh Mkhitaryan na Ander Herrera walihudhuria tukio la wadhamini muda mfupi baada ya kuwasili kwenye hotel waliofikia timu hiyo.
Manchester united itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Borrusia Dortmund ambayo itamkutanisha Henrikh Mkhitaryan na wachezaji wenzake wa zamani siku ya ijumaa.
Mourinho alipanga orodha ya wachezaji atakaokwenda nao nchini lakini alimwacha mshambuliaji kinda wa Manchester united James Wilson ambaye bado mustakabali wake haujafahamika tangu aliposajiliwa Zlatan Ibrahimovic.

Comments
Post a Comment