Manara: Maneno ya Jerry Muro balaa


Ofisa habari wa timu ya Simba Haji Manara amesema maneno ya Jerry Muro ndiyo yanayowafanya mashabiki wa Simba washindwe kuisapoti Yanga kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Manara aliongea maneno hayo ikiwa ni sehemu ya utani baada ya kutambelewa nyumbani kwake na baadhi ya wanachama wa Yanga ambao waliongoza na Ofisa habari huyo.

"Mdomo wa mtoto wa kichaga ndiyo unawatia uchungu mashabiki wa simba wasishangirie wapinzani wao kwenye michezo ya kimataifa." Alisema Manara huku akicheka

Wanachama hao walifika kumtakia pole na kuwasilisha michango yao kwa ajili ya kumsampoti Haji Manara anayesumbuliwa na macho kwenda kutibiwa India.


Comments