Manula apata mbabe Azam


Kipa namba moja wa timu ya Azam Aishi Manula amepata mpinzani golini baada ya Azam kumleta kipa wa Ivory Coast Daniel Yeboah.

Yeboah 31, alitua jana ili kukamilisha taratibu za mwisho za usajili katika timu ya Azam ambao wanataka kujiweka sawa baada ya kupotea kwenye ubingwa kwa miaka miwili.

Kipa huyo amewahi kutamba akiwa na Asec Mimosa na pia amewahi kuchezea timu ya Dijon inayoshirki ligi daraja la pili nchini Ufaransa.

Comments