Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa Blaise Matuidi alipanda kuelekea England ili kufanya mazungumzo na timu ya Manchester united.
Mourinho anavutiwa na mpango wa kkumsajili nyota huyo wa Paris Saint Germain (PSG) kutokana na kuwa kwenye kiwango bora kwa muda wote.
Matuidi 29, alikuwa kenye mapumziko mafupi baada ya Ufaransa kufuzu hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya UEFA Euro inayoendelea nchini humo na kutumia nafasi hiyo kuelekea England kufanya mazungumzo.
Mchezaji huyo amekuwa muhimili katika timu ya PSG na sasa anaendelea kufanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

Comments
Post a Comment