Mshambuliaji Burundi na klabu ya Vital O' Laudit Mavugo anatarajiwa kusaini Simba muda wowote kuanzia sasa.
Simba ipo kwenye hatua ya mwisho ya kukamilisha dili la mshambuliaji huyo ambaye ilimkosa mwaka jana baada ya kuongeza kwa dau la usajili la mcheazaji huyo.
Mavugo alisema kuwa anasubiri Simba imtumie tiketi kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kusaini msimbazi kwa makubaliano ya mkataba wa miaka 2.
"Nipo kwenye mipango ya kuja Simba muda wowote kuanzia sasa mambo yakienda vizuri nitasaini miaka 2." Alisema Mavugo.

Comments
Post a Comment