Mavugo azitia vitani Simba, Gor Mahia


Baada ya Simba kutangaza kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burundi Laudit Mavugo ambaye amemaliza mkataba wake na Vital O' mabingwa wa Kenya Gor Mahia nao wameingilia mchakato huo.

Simba iliandaa dau nono la kumshawishi mshambuliaji huyo kutua msaimbazi lakini sasa kutakuwa na ushindani mkubwa wa kumwania Mavugo baada ya Gor Mahia kuonesha nia ya kumsajili.

Gor Mahia ambao ni mabingwa mara 3 mfululizo wanataka kuimarisha timu yao  kutokana na kushiriki michuano ya kimataifa na ile ya ndani na wanaona mrundi huyo ni sehemu ya mafanikio kwao.

Simba inataka kurejesha makali yake baada ya kupoteza ubingwa kwa miaka minne sasa na imepanga kusajili wachezaji bora ambao watarajesha heshima ya timu hiyo na Mavungo amekuwa kwenye mipango yao kwa muda mrefu sasa.


Comments