Mayanga Rasmi Mtibwa

Kocha na mchezaji wa zamani wa klabu ya wakata miwa wa Mtibwa, Salum Mayanga amerejea kukinoa kikosi hicho baada ya kocha wa wana wa turiani Mecky Mexime kuamia kwa ndugu zao wakata miwa wa Kagera.

Afisa habari wa timu hiyo Thobias kifalu amesema wamempa jukumu Mayanga kutoka na uwezo wake na pia ni mwalimu ambaye ana historia na klabu hiyo.

Mayanga msimu uliopita alikuwa na timu ya prisons ya jijini mbeya akiwawezesha kuwa moja ya timu zilizofanya vizuri, ni miongoni mwa makocha waliojumuishwa kwenye kuwania tuzo ya kocha bora wa msimu wa ligi kuu ya vodacom kwa msimu wa 2015/2016.

Hii ni mara ya pili kwa Mayanga kuifundisha klabu ya Mtibwa Sugar kama kocha mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa  2008/09 na 2009/10 ambapo aliweza kuipatia klabu ya mtibwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaaa kombe la Tusker, Kombe la Mapinduzi  na Ngao ya Jamii. 

Kabla ya kuwa  kocha mkuu wa timu hiyo, Mayanga alikuwa kocha m
saidizi wa kikosi hicho cha wakata miwa wa Turiani chini ya makocha kadhaa wakiwemo Twahir Muhidin, Tom Olaba, James Sianga na Abdallah Kibaden.

Mayanga kabla hajawa  mwalimu wa soka  alikuwa ni mchezaji na nahodha wa mtibwa katika kipindi cha miaka ya tisini na ni miongoni mwa makocha walioipandisha daraja klabu ya Mtibwa kwenda ligi daraja la kwanza kabla ya kubadilishwa jina na kuwa ligi kuu.

.

Comments