Mayanja mambo safi Simba.


Baada ya kuwa na mashaka juu ya nini kitatokea kwa kocha wa Simba Jackson Mayanja hatimaye kocha atabaki Msimbazi.

Mayanja amefanya mazungumzo na Simba na atabaki kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo akimsaidia Joseph Omog.

Mayanja ameanza kuonekana mazoezi ikiwa ni dalili tosha kuwa mazungumzo katika ya kocha huyo na uongozi wa Simba yanakwenda vizuri.

Hivi karibuni kocha huyo alihusishwa na mpango wa kurudi katika timu yake ya zamani ya Kagera Sugar lakini sasa mambo yamekuwa tofauti baada ya Omog kutoa tamko kuwa anamwitaji kocha huyo.

Comments