Mayanja: Simba hii kiboko


Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kuwa mazoezi ya mwalimu Joseph Omog yataifanya Simba itishe msimu ujao.

Kocha huyo amesema kuwa wamekinoa kikosi hicho ipasavyo na hali ya mazoezi kwa wachezaji imeongezeka na wengi wa wachezaji wamekuwa kwenye kiwango bora.

Kocha huyo aliongeza kuwa wapinzani wa Simba wajiandae kwa kuwa ana imani kwa mbinu wanazotoa hakuna wa kushindana na kikosi chao.

"Ukijumlisha mbinu zangu na za mwalimu Omong nadhani sisi ni tishio kwa sasa, nadhani mataji yatarejea hapa msimu ujao." Alisema Mayanja

Comments